11 wapona, vifo 4, wagonjwa wapya 29 Tanzania
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametangaza ongezeko la wagonjwa 29 wa COVID-19 ambapo wote ni Watanzania, 26 wapo Dar es Salaam, wawili wapo Mwanza na mmoja yupo Kilimanjaro, hali inayopelekea Tanzania kuwa na jumla ya visa 88.