"Wagonjwa wa Corona walitaka kutoroka" - DC Ilala
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amesema kuwa bado hajapata taarifa za waathirika wa Virusi vya Corona, waliopo katika kituo maalum katika Hospitali ya Amana, kama wametoroka na kurejea makwao ila anachojua walikuwa wanatishia kuondoka kwa madai ya kuwa hali zao kiafya ni nzuri.