Huyu ndiye Balozi Dkt Augustine Mahiga
Balozi Dkt Augustine Mahiga alizaliwa Agosti 28, 1945, Kijiji cha Tosamaganga mkoani Iringa, alisoma elimu yake ya Msingi na Sekondari hapa nchini na baadaye mwaka 1968, alijiunga na Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, DSM na kuhitimu Shahada ya Sanaa akibobea kwenye Elimu mwaka 1971.