Uhalifu wadhibitiwa ndani ya ziwa Victoria
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kudhibiti matukio mbalimbali ya kihalifu yanayojitokeza ndani ya Ziwa Victoria, vikiwemo vitendo vya uvuvi haramu na uporaji wa kutumia silaha, kufuatia doria zinazoendelea kufanywa na askari wa jeshi hilo kwa nyakati tofauti.

