China kuwapa ruzuku watoto chini ya miaka 3
Serikali ya China inapanga kuwapa wazazi ruzuku ya kila mwaka ya yuan 3,600 sawa na Shilingi 1,285,000 kwa kila mtoto aliye chini ya umri wa miaka mitatu, kama hatua ya kuchochea ongezeko la viwango vya uzazi ambavyo vimeshuka nchini humo.