Stars matumaini makubwa kufuzu AFCON 2025

Taifa Stars inashika nafasi ya pili kwenye kundi H nyuma ya Congo DRC yenye alama 9 ikiwa imecheza michezo mitatu sawa na idadi ya Stars iliyojikusanyia alama 4 iliyo nafasi ya pili. Timu ya taifa ya Tanzania imepoteza mchezo ugenini dhidi ya Congo DRC kwa goli 1-0, mchezo wa marudiano wa kufuzu michuano ya AFCON 2025 unatarajiwa kuchezwa Oktoba 15, 2024 Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam.
Timu ya taifa ya Tanzania imebakiza michezo mitatu dhidi ya Congo DRC, Ethiopia na Guinea na itapaswa kushinda michezo miwili inayofuatia ya nyumbani ili kuweza kufuzu kucheza michuano ya AFCON itakayofanyika nchini Morocco mwaka 2025