Mtendaji mbaroni tuhuma rushwa ya laki tatu
TAKUKURU wilaya ya Bukombe mkoani Geita, imemfikisha mahakamani Rashid Musalika ambaye ni Afisa Mtendaji wa kata ya Runzewe Mashariki kwa tuhuma za kujipatia shilingi laki tatu kutoka kwa wafugaji wa ng'ombe ili aweze kuachilia ng'ombe zao zilizokuwa zimelisha kwenye shamba la mkulima.