Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuongeza muda wa kuandikisha watu katika daftari la kudumu la wapigakura na kuongeza mashine za BVR zinzazotumika kuandikisha watu kwa ajili ya kuharakisha zoezi hilo.
Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wa chama hicho Dkt Wilibroad Slaa mara baada ya kutembelea vituo mbalimbali vya undikishaji ambapo amebaini changamoto nyingi wanazokabilia nazo wananchi katika kuajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ikiwemo upungufu wa machine.
Dkt Slaa ameitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuhakikisha inaongeza mashine kwa ajili ya kuharakisha zoezi hilo linalondelea mkoani Kagera.
Dk Slaa pia ameongeza kwa kuitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuweka mambo wazi na kuacha masuala ya usiri juu ya zoezi hilo la uandikisha wapiga kura badala yake wawaweke wazi watanzania ili waweze kutambua umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza kujiandikisha wamesema wamekuwa wakikabaliana changamo mbalimbali huku wengine wakisema kuwa wamekuwa wakipanga foleni tangu juzi lakini hawajafanikiwa kujiandikisha kutokana na uchache wa mashine zilizopo na kusababisha msongamano mkubwa wawatu.