Thursday , 7th May , 2015

Michuano ya Klabu bingwa Taifa ya mpira wa kikapu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo kesho uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Kamishna wa Ufundi na Uendeshaji Mashindano wa TBF, Manase Zablon amesema walitarajia kuwa na timu 30 ambapo 15 zikiwa za wanaume na 15 za wanawake lakini mpaka sasa timu zilizothibitisha ushiriki ni 29.

Manase amesema, ratiba ya michuano hiyo inatarajiwa kupangwa usiku wa leo katika kikao cha maandalizi huku dirisha la uhakiki wa timu shiriki likiwa limeshafungwa tangu Mei 02 mwaka huu.