Saturday , 18th Apr , 2015

Pamoja na jitihada za serikali na wadau wa elimu katika kupunguza utoroshwaji wa watoto wa kike mashuleni zinazochangiwa na mila potovu imebainika kuwa wanafunzi wengi kwa sasa wanaacha shule kutokana na kurubuniwa na vijana na wazee.

Wanafunzi wa moja ya shul;e za Sekondari Arusha wakionyesha vitabu walivyokabidhiwa kama Msaada.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa shule ya sekondari Kifaru Abdallah Mwomboke iliyopo katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro ambaye amesema hali hiyo imewapelekea wao kama shule kuona umuhimu wa kujenga mabweni kwa ajili ya watoto wa kike kwa sababu wengi wameshindwa kuendelea na masomo shuleni baada ya kuingizwa katika mahusiano na wanaume hali ambayo inawawia vingumu kuweza kumudu masomo.

Awali katika ghafula fupi ya kuunga mkono jitihada zashule hiyo kumwezesha mtoto wa kike kujiendeleza meneja mauzo wa benki ya kibiashara ya afrika CBA Solomon Kawiche na ambayo imetoa mchango wa shilingi millioni tano kwa ajili ya ujenzi huo amesema wao kama benki wameona umuhimu wa kumweshesha mtoto wa kike kutikana na majukumu mengi yanayowawia watoto hao katika

Kwa upande wa wanufaika wa mchango huo ambao ni watoto wa kike mwanafuzi Lema Emmanuel pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa kuona umuhimu wa kuchangia ujenzi huo pia ameiomba jamii kuweza kutia jitihada za ziada katika kuweza kuendeleza elimu hapa nchini na kuendeleza maendeleo katika jamii.