Friday , 10th Apr , 2015

Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania Mathias Chikawe leo amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania imejipanga kulinda usalama wa raia wake dhidi ya ugaidi kote nchini.

Waziri Chikawe amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotaka kujua usalama wa nchi kwa sasa, kutokana na mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea kwa nchi za jirani siku chache zilizopita.

Aidha Waziri Chikawe ameongeza kuwa vita hii ya ugaidi ni ya kila mtu na ni jukumu la watu wote kutoa taarifa wanapoona kitu tofauti hasa uwepo wa wageni nchini na kuwatilia mashaka.

Akizungumzia Mitandao Waziri Chikawe amewataka wananchi kuacha mara moja tabia yakutumiana jumbe zenye mambo ya vitisho vya ugaidi kwenye mitandao kwani kwa kufanya hivyo itawapa wasiwasi mkubwa baadhi ya wananchi na kuwafanya wasifanye kazi zao kwa umakini na pia serikali haitazipuuzia habari hizo na kuongea kuwa atazifanyia kazi kwa umakini zaidi.