Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Juma Zuberi Homera akizungumzia mafanikio ya programu ya "Sema na Waziri," iliyozinduliwa tarehe 17 Machi, 2026, amesema programu hiyo imekuwa chombo muhimu cha kuunganisha wananchi na Serikali.
Waziri Homera ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa programu hiyo jumla ya malalamiko 67 yamepokelewa, kati ya hayo malalamiko 38, sawa na asilimia 56.7, yameshughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi, huku 29 sawa na asilimia 43.3 yakiendelea kufanyiwa kazi.
Aidha amebainisha kuwa migogoro ya ardhi imeongoza kwa asilimia 31.3, ikifuatiwa na migogoro ya kazi na ajira asilimia 19.4, madai asilimia 13.4, mirathi asilimia 7.4, maombi ya msaada wa kisheria asilimia 7.4, na asilimia 21.1 masuala mengineyo yakiwemo jinai, utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, maombi ya nyongeza ya muda na ukatili wa kijinsia.
"Ninawahakikishia wananchi kwamba hakuna malalamiko yatakayopuuzwa,nitapokea malalamiko mara mbili kwa kila mwezi na kutoa mrejesho wa wazi," amesisitiza Waziri Homera.
Waziri amehimiza wananchi wote, hasa wanaoishi maeneo ya pembezoni, kuendelea kutumia jukwaa hilo kuwasilisha maoni na changamoto zinazowakabili.



