Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, anatarajiwa kuwasili nchini, kesho Jumamosi, tarehe 07 Februari, 2026 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Katika ziara hii, Rais Museveni atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mazungumzo yao yatajikita kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizi mbili, na kujadili masuala muhimu ya kikanda na kimataifa.
Miongoni mwa masuala yatakayozungumzwa ni suala la nishati, hususan Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP), ambao unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa nchi zote mbili na kanda kwa ujumla.
Rais Museveni na Rais Samia pia watazungumza na vyombo vya habari kuhusu mazungumzo yao.




