Mtu mmoja ambae majina lake bado hayajafahamika amekutwa amefariki dunia ndani ya nyumba ya kulala wageni inayofahamika kwa jina la Kisenga iliyopo eneo la Tawi la Yanga,Kata ya Mazimbu,Manispaa ya Morogoro alipokuwa amelala usiku wa kuamkia leo.
EATV,imefika katika eneo la tukio na kuzungumza na baadhi ya mashuhuda ambao wameeleza EATV kuhusu tuki hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amefika katika eneo hilo la tukio na kusema kuwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mtu huyo amejiua kwa kujichana koromeo.
"Nimekuja kukagua tukio hili ambalo mtu mmoja ambae bado majina yake tunayafanyia uchunguzi hatujaweza kuyapata vizuri,ni mgeni alikuwa amelala chumba namba 106 ambapo asubuhi ilibainika kuna damu zinachuruzika kutoka kwenye chumba alichokuwa amelala kuanzia hapo tumepata taarifa na ndio tumekuja kuanza uchunguzi"amesema SACP Alex Mkama Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro




