Akizungumza na East Africa Radio, Najaha Bakari amesema, mgogoro huo umesuluhishwa na kamati ya usuluhishi ya nidhamu na rufaa ya BMT, Jamal Rwambow ambapo amesema mgogoro huo umetokana na TTA kukosa kingozi wa ngazi ya juu ambaye angeongoza chama hicho na kuweza kuepusha hata migogoro iliyojitokeza.
Najaha amesema, katika kikao hicho, TTA walikubali kuomba msamaha ambapo wametakiwa kuomba msamaha kwa maandishi pamoja na kufanya mabadiliko ya katiba na wawasilishe kwa msajili.