Friday , 12th Dec , 2025

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake baada ya uchunguzi kukamilika.

Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam limethibitisha kumshikilia Geofrey Mwambe kwa tuhuma za jinai ambazo bado zinafanyiwa uchunguzi.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam iliyotolewa leo Disemba 12 imesema Mwambe alikamatwa mnamo Disemba 7, 2025 majira ya usiku katika eneo la Tegeta, Manispaa ya Kinondoni.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake baada ya uchunguzi kukamilika.

Tamko la polisi limekuja siku moja baada ya Wakili wa Mwambe, Hekima Mwasipu kuiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa amri ya kupewa dhamana au kufikishwa Mahakamani kwa mteja wake katika maombi yenye namba 289778 ya mwaka 2025 dhidi ya wajibu maombi watatu Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na ZCO wa Kanda ya Dar es Salaam.