Monday , 24th Nov , 2025

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, amemshauri kocha wa Liverpool Arne Slot kuchukua uamuzi wa kumtema Mohamed Salah kwenye kikosi chake cha kwanza.

Arne Slot, Salah na Wyne Rooney (kwenye duara)

Rooney ametoa ushauri huo, kupitia kipindi chake cha podcast, akibainisha kuwa mchango wa Salah katika mechi dhidi ya Nottingham Forest ulikuwa hafifu, huku mchezaji huyo akishindwa kufunga na kutoa pasi ya bao.

Rooney, ambaye ameshinda Ubingwa wa Ligi Kuu mara tano, amebainisha kuwa Slot anaposhindwa kuchukua uamuzi huo, inaweza kuathiri morali ya wachezaji waliokuwa benchi. Kwani mchezaji anaposhindwa kuonyesha bidii, wachezaji wengine wanaweza kupata hisia potofu juu ya jukumu lao na mchango wao katika timu.

Salah, mwenye umri wa miaka 33, aliwahi kuwa mwanasoka wa historia ya Premier League kufikia rekodi ya juu ya mabao na pasi za mabao na kupata tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu, lakini kwa sasa Liverpool inakabiliwa na changamoto kutokana na matokeo duni ya hivi karibuni.

Liverpool kwa sasa ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya EPL, ikiwa na pointi 18, baada ya kucheza mechi 12.