Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limethibitisha kutokea kwa tukio la mauaji ya Maria Salvatory lilitokea Novemba 17, 2025 katika Kata ya Lwamgasa Wilaya ya Geita.
Kupitia taarifa ya Jeshi hilo iliyotolewa jana Novemba 19, 2025, chanzo cha kifo hicho kinadaiwa kuwa ni wivu wa Chanzo cha tukio hilo kimetajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Taarifa ya Polisi imedai kwamba Maria aliuwawa baada ya kushambuliwa kwa kupigwa na kitu butu kichwani na kuchomwa kitu chenye ncha kali sehmu mbalimbali za mwili wake, tukio ambalo lilitekelezwa na mumewe Mayala Juma.
Baada ya tukio hilo Mayala alijifungia chumbani na kunywa sumu aina ya "Synom Crown" pamoja na dawa nyingine katika jaribio la kutaka kujiua na licha ya kukimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Geita Mayala alipoteza maisha Alfajiri ya Novemba 18, 2025.
Taarifa ya Jeshi la Polisi imebainisha kwamba baada ya miili hiyo kufanyiwa uchunguzi imekabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za Mazishi. Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limeendelea kuwasihi Wananchi katika mkoa huo kutatua migogoro mapema ili kuepusha madhara yanayoweza kuepukika.
