Friday , 29th Aug , 2025

Afrika Kusini imeendelea na maandalizi zikiwa zimesalia siku 100 kabla ya Mkutano wa kwanza Kihistoria wa Viongozi wa G20 kufanyika katika ardhi ya Afrika mjini Johannesburg mwezi November.

Afrika Kusini ambayo ilichukua Urais wa G20 Disemba Mosi, 2024 itaachia nafasi hiyo kwa nchi nyingine itakayochaguliwa. Swali kuu ambalo wengi wanajiuliza ni iwapo Rais wa Marekani Donald Trump atahudhuria kwani ameonyesha kutokubaliana vikali na sera za Afrika Kusini hasa mageuzi ya ardhi na kuashiria kwamba anaweza kutuma mwakilishi badala yake.

Licha ya hayo, Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini , Ronald Lamola amesema  mwaliko wa Afrika Kusini unaendele kusimama. "Tutaendelea na Mkutano wa Viongozi wa G20 pamoja na au bila Rais Trump. Ni hali isiyotabirika."

Mikutano iliyosalia ya mawaziri mwezi Septemba itaweka sauti kwa Tamko la Viongozi wa Johannesburg, lililoegemezwa kwenye Mshikamano, Usawa, na Uendelevu. Mfumo huu unalenga kusaidia kuweka mwelekeo wa uchumi wa kimataifa kwa mkutano huo.

Masuala muhimu yatakayojadiliwa  ni pamoja na ukosefu wa usawa wa kimataifa na mizigo ya madeni huru. Ili kukabiliana na hili, Rais Cyril Ramaphosa amezindua kikosi kazi cha G20, kinachoongozwa na mwanauchumi aliyeshinda Tuzo ya Nobel Joseph Stiglitz, kuchunguza tofauti za utajiri na kupendekeza suluhu zinazoweza kuchukuliwa.