Saturday , 16th Aug , 2025

Zoezi la kuwaokoa watu waliofukiwa na kifusi katika mgodi wa Dhahabu Nyandolwa kata ya Mwenge Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga linaendelea huku ikidaiwa kuwa bado watu wawili wakifariki dunia na wengine  20 bado wamekwama ardhini 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro  amethibitisha  kwa njia ya simu  na kuwaeleza waandishi wa habari waliopo eneo la tukio kuwa mwili mwingine mmoja wa kijana  Magumba Ngondi (28) umeopolewa huku akiwa  amefariki.

 "Mwili wa marehemu ulioopolewa leo  umehifadhiwa  katika chumba cha maiti katika hospitaliya wilaya iliyopo Iselamagazi, lakini pia  zoezi la uokoaji linaendelea," amesema Mtatiro

Amesema vikosi vya uokoaji  tangu  juzi viliungana vikiwemo kikosi cha zimamoto, Msalaba mwekundu na Uokoaji kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu  

Katika tukio hilo jumla ya watu 25 walibainika kufukiwa na kifusi katika mgodi huo  mpaka sasa watu watatu wameokolewa na hali zao ni nzuri,  huku wawili ambao ni  Emanuel Kija na Magumba Ngondi wamefariki #EastAfricaTV