
Video inayomuonyesha msichana akizabwa kofi, kupIgwa teke na kulazimishwa kupiga magoti na wanafunzi wengine watatu ilisambaa katika mji wa Jiangyou katika mkoa wa Sichuan wiki iliyopita.
Polisi wanasema washukiwa watatu wote wasichana, wenye umri wa miaka 13, 14 na 15 - wawili kati yao walikuwa wamepelekwa "shule maalum ya urekebishaji tabia".
Taarifa za tukio hilo zimeendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, baadhi ya watu wakilalamika kuwa adhabu iliyotolewa kwa wasichana hao ni nyepesi - hasa baada ya madai kuwa msichana huyo alionewa kwa muda.
Katika mfululizo wa video, zilizorekodiwa na washambuliai hao, mwathiriwa anasikika akisema atapiga ripoti polisi baada ya kupigwa viboko mara kwa mara huki mmoja wa wasichana wanaomshambulia akasema hawakuogopi.
Mwingine alisema ashawahi kufikishwa kituo cha polisi zaidi ya mara 10, na kudai kuwa aliachiliwa kwa chini ya dakika 20.
Tukio hilo limezusha wimbi la hasira za umma mtandaoni na maandamano yalizuka nje ya ofisi za serikali ya mtaa huko Jiangyou.
Zaidi ya watu 1,000 walikusanyika barabarani tarehe Agosti 4 na kusalia mitaani hadi usiku wa manane, kulingana na wamiliki wa maduka ya ndani.