
Kampeni ya ‘Badilika Tokomeza Ukatili’ imezinduliwa katika maandamano yaliyoongozwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima pamoja na wananchi katika uwanja wa Mwanga Center Kigoma.
Kampeni hiyo iliyozinduliwa leo Julai 28, 2025, ni mwendelezo wa juhudi za kuhamasisha jamii kutambua, kukemea na kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ukatili hususani kwa wanawake na watoto.
Katika chapisho aliloliandika kwenye mtandao wake wa Instagram, Waziri Gwajima amesema kampeni hiyo inalenga kukabiliana na mila na desturi hatarishi pamoja na ukatili wa kijinsia.
Uzinduzi huo umehudhuliwa pia na viongozi mbalimbali wa serikali na mashirika ya kiraia,wajassiriamali wanawake na vikundi mbalimbali vya vijana.