Wednesday , 23rd Jul , 2025

Watu 125 wanatuhumiwa kuhusika na makosa mbalimbali wakiwemo wenye makosa ya kutumia dawa za kulevya na kusambaza,pamoja na wizi wa mali mbalimbali katika kipindi cha kuanzia mwezi juni 27,2025 hadi julai 22,2025 .

Watu 125 wanatuhumiwa kuhusika na makosa mbalimbali wakiwemo wenye makosa ya kutumia dawa za kulevya na kusambaza,pamoja na wizi wa mali mbalimbali katika kipindi cha kuanzia mwezi juni 27,2025 hadi julai 22,2025 .

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akizungumza na vyombo vya habari leo Julai 23, 2025, amesema watuhumiwa hao walikamatwa wakati jeshi hilo likifanya operesheni iliyolenga kubaini na kuzuia uhalifu.

Amesema  katika operesheni hizo, dawa za kulevya zilizokamatwa ni pamoja na bhangi gramu 2,261 mirungi kilo 29 pamoja na pombe ya moshi lita 142. bajaji moja ,runinga saba mbati 16, nondo vipande 17 vitanda vinne pikipiki mbili, redio nane na risasi moja ya silaha ndogo.

Aidha amesema jumla ya kesi 25 zimepata mafanikio ambapo kesi mbili za kulawiti washitakiwa wawili wamehukumiwa kifungocha maisha jela, kesi mbili za kubaka, ambapo washitakiwa wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

Amesema kesi nyingine ya kuvunja nyumba usiku na kuiba washitakiwa watano wamehukumiwa kifungo cha miezi miwili mpaka miaka minne jela, kesi nane za wizi washitakiwa 21 wamehukumiwa kifungo cha miezi miwili mpaka miaka mitatu jela.

Magomi amesema jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kupitia kikosi cha usalama barabarani limeendelea na operesheni mbalimbali dhidi ya madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani ambapo limefanikiwa kukamata jumla ya makosa 5,759 na katika makosa hayo makosa ya magari ni 4,557 huku makosa yanayohusika na pikipiki yakiwa 1,202.

Kamanda Magomi amesema kuwa operesheni hizo zinaendelea kwa lengo la kuhakikisha jamii inakuwa salama dhidi ya vitendo vya uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya. 

Hata hivyo kamanda amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na vitendo viovu vinavyofanyika katika maeneo yao na kuhakikisha usalama upo.