
Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 22 mkataba wake wa awali ulikuwa unatamatika 2027 na kabla ya kusaini mkataba huo alikuwa akihusishwa kutimkia FC Barcelona kwa mabingwa wa La Liga 2024-2025.
Baada ya mkataba huo Nico Williams akihitaji kuondoka atatakiwa kulipa zaidi ya euro milioni 90 ambayo ni zaidi ya bilioni 27 kwa shilingi ya Tanzania.
Nico ambaye ameisaidia Hispania kushinda kombe la EURO 2024 akifunga katika ushindi wa 2-1 walioupata mbele ya England. Pia msimu katika ligi ya La Liga amechangia upatikanaji wa mabao 10 katika michezo 29 aliyocheza.