
Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi wa picha mjongeo ambayo inaonekana kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha kijana aliyeefungwa mikono huku akipigwa kwa fimbo.
Tukio hilo lilikuwa Juni 26, 2025 na kutokana na kushambuliwa huko kwa kipigo, kijana huyo anayejulikana kwa jina la Enock Thomas Mhangwa alifariki Dunia.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wanaodaiwa kuhusika katika mauaji hayo, ambao ni Ferdinand Antony Masembo Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Liyobahika na Hussein Ally Madebe huku Watuhumiwa wengine wanaendelea kutafutwa akiwepo Mtendaji wa kijiji cha Uyovu na Mgambo wawili wambo wamekimbia.
Jeshi la Polisi limetoa wito kwa watu wengine wakuchukulia sheria mkono, waache kwani halitasita kuwakamata ili hatua za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake kama itakavyo fanvika kawa wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji hayo.