Friday , 4th Jul , 2025

Klabu ya soka ya Liverpool imetoa taarifa kwa umma kuwa itastaafisha jezi nambari 20 aliyokuwa anaitumia winga wa Ureno Diogo Jota, ambaye alifariki dunia kwa ajali ya gari (Lamborghini) akiwa na mdogo wake André Silva siku ya Alhamis huko Zamora nchini Uhispania.

Jota, ambaye alijiunga na klabu hiyo mwaka wa 2020 akitokea Wolves, alicheza mechi 182, alifunga mabao 65, na kutoa asisti 26 atazikwa Jumamosi Julai 05/2025 Saa 4 asubuhi nchini Ureno.

Liverpool inastaafisha jezi namba 20 kwa heshima ya Diogo Jota, hivyo hakuna mchezaji wa Liverpool atakayeweza kuvaa namba hiyo.