Wednesday , 18th Jun , 2025

Klabu ya Liverpool inataka kufungua mazungumzo ya moja kwa moja kwa mchezaji wa Newcastle Anthony Gordon. Kuna uwezekano wa mchezaji huyo akajiunga na Miamba hao wa Premier League msimu huu wa Joto.

Anthony Gordon

Huenda mazungumzo yakaanza wiki hii au wiki ijayo, hii yote ni kutokana na wachezaji wa Liverpool Luis Diaz na Diogo Jota ambao wanaweza kuondoka katika dirisha hili la kiangazi.

Washambuliaji hao wanalewa kuwa nafasi yao kubwa ni kuondoka klabuni hapo, na Liverpool imemuona Anthony Gordon kuwa sehemu ya mpango huo.

Pia Liverpool inapanga kufanya usajili wa washambuliaji wawili na kiungo mkabaji mmoja pamoja na beki wa kati mmoja kabla dirisha kubwa halijafungwa mwezi August.