Wednesday , 18th Jun , 2025

Imeelezwa kuwa Utumiaji wa bangi huongeza hatari ya kufa kutokana na ugonjwa wa moyo na hii ni kutokana na  na uchambuzi mpya wa data ya matibabu iliyohusisha watu milioni 200 wengi wao wakiwa kati ya umri wa miaka 19 na 59

Utafiti uliochapishwa katika jarida maarufu la magonjwa ya  Moyo umeeleza kuwa ikilinganishwa na wasiotumia, wale waliotumia bangi pia wana hatari kubwa ya 29% ya mshtuko wa moyo na hatari kubwa ya 20% ya kiharusi

Daktari wa watoto na Profesa wa kliniki inayohusika na takwimu za magonjwa katika Chuo Kikuu cha California, San Francisco Dk. Lynn Silver, amesema kuwa Huu ni moja ya tafiti kubwa zaidi hadi sasa unaohusu uhusiano kati ya bangi na ugonjwa wa moyo, na unaibua maswali mazito kuhusu dhana kwamba bangi huwa na hatari ndogo kwa moyo na mishipa