Wednesday , 18th Jun , 2025

Muongozaji na muigizaji maarufu wa filamu Marekani Tyler Perry ameingia kwenye tuhuma za unyanyasaji wa kingono ambazo zimetolewa na mmoja wa waigizaji wake katika series yake ya The Oval aitwaye Derek Dixon

Muigizaji huyo amemfungulia mashitaka Tyler Perry huku akitaka kulipwa fidia ya dola milioni 260 ambayo ni sawa na bilioni 680 kwa pesa za kitanzania

Timu ya wanasheria wa Nguli Tyler Perry imekanusha madai hayo na kusema kuwa lengo  la mashitaka hayo ni kutaka kumpunguza nguvu Muigizaji huyo

Ikimbukwe kuwa wasanii Diddy ,R Kelly wanakabiriwa na kesi za aina hii jambo ambalo limewafanya baadhi ya wadau kuanza kufikiria ya kuwa huenda Perry na yeye akakumbwa na yaliyowakuta Diddy na R Kelly