Friday , 13th Jun , 2025

Mabingwa wa Premier League Liverpool wamekubali kutoa pesa paundi £116m kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Florian Wirtz kutoka Bayer Leverkusen.

Florian Wirtz

Ada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 itatolewa kwa awamu mbili ikiwa ni £100m na ​​nyongeza ya £16m. Uhamisho huo, utakuwa rekod

Mshambulizi wa Uruguay Darwin Nunez alisajiliwa kutoka Benfica kwa ada ya awali ya £64m na kupanda hadi £85m kama nyongeza, huku wakilipa £75m kumsajili beki wa kati Virgil van Dijk kutoka Southampton mwaka 2018.

Rekodi ya Uingereza kwa ada ya awali inasalia kuwa Chelsea ya pauni milioni 107 walipomsajili kiungo wa kati raia wa Argentina Enzo Fernandez kutoka Benfica mwaka 2023. Chelsea pia ilimnunua kiungo wa Brighton Moises Caicedo kwa ada ya awali ya £100m, ambayo inatajwa kuwa itapanda hadi £115m.