Friday , 13th Jun , 2025

Ndege ya Air India iliyokuwa inatoka Phuket nchini Thailand kuelekea mji mkuu wa India New Delhi imelazimika kutua kwa dharura katika kisiwa hicho kutokana na kupokea taarifa za tishio la bomu katika ndege hiyo

Ndege hiyo ilipaa kutoka uwanja wa ndege wa Phuket kuelekea mji mkuu wa India saa tatu na nusu asubuhi leo Ijumaa, lakini ilizunguka Bahari ya Andaman na kutua tena kwenye kisiwa cha kusini mwa Thailand

Afisa mmoja wa viwanja vya ndege vya Thailand amesema kuwa abiria wote 156 waliokuwa kwenye ndege hiyo ya AI 379 walisindikizwa kutoka kwenye ndege hiyo wakiwa salama

Hata hivyo walinda usalama wa Thailand walifika haraka, wakaikagua ndege nzima, hakuna bomu wala vilipuzi vilivyopatikana na tayari uchunguzi rasmi wa tukio hilo umeanza