Tuesday , 20th May , 2025

Man City wamejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili nyota wa Bayer Leverkusen Florian Wirtz anayetajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 126 na kuziacha Liverpool na Bayern Munich zikipigania kumnasa nyota wa Ujerumani.

Florian Wirtz - Nyota wa Bayer Leverkusen

Sababu za msingi kwa Man City kujiondoa ni gharama kubwa zilizotajwa kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 22. Wirtz, ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kikosi cha Leverkusen msimu uliopita, alionekana kama mrithi wa Kevin De Bruyne anayeondoka Man City.

Magoli 18 na asisti 20 yalimfanya chipukizi huyo kutambulika kimataifa msimu uliopita, na msimu huu amefunga mabao 16. Kikosi cha Pep Guardiola si mara ya kwanza kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwanunua wachezaji wenye gharama kubwa ikiwemo Harry Kane wakati Daniel Levy  ada ya pauni milioni 150 na badala yake wakalipa pauni milioni 100 kwa Jack Grealish na pauni milioni 51 Erling Haaland.