Thursday , 15th May , 2025

Magari yanayosafiri kutoka Bukoba mkoani Kagera kuelekea mikoa mingine, yamekwama katika eneo la Kyetema kufuatia kuharibika kwa barabara ya dharura inayotumiwa na magari hayo na kusababisha adha kwa abiria huku ikielezwa kuwa uharibifu huo umetokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Magari yaliyokwama barabarani

Baadhi ya abiria wamesema kuwa magari kadhaa yameshindwa kupita katika eneo hilo baada ya barabara hiyo kujaa tope na maji, hali iliyosababisha msongamano mkubwa wa vyombo vya usafiri.

"Mvua iliyonyesha kuanzia saa 7:00 usiku imesababisha barabara kuharibika na magari yaliyopo hapa ni ya kuanzia muda huo, imetuletea shida watu wanakwama kusafiri wengine tunaenda kazini," amesema Jonson Mulokozi

Mpaka sasa juhudi za kuhakikisha magari yanapita zinaendelea huku tayari magari yameanza kupita chini ya uangalizi wa mkandarasi aliyepewa ujenzi wa daraja eneo hilo huku jeshi la polisi wakizidisha ulinzi kutokana na msongamano uliopo