Wednesday , 14th May , 2025

Msanii ibraah amefunguka kilichozungumwa siku ya leo baada ya kuitwa na walezi wao Basata siku ya leo kwaajili ya kuzungumzia hili linaloendelea kwasasa kati yake na Label yake ya Konde Gang

Pichani ni Harmonize na Ibraah

Baada ya Chinga kutoka kwenye kikao hicho amezungumza na waandishi wa habari na ameweka wazi kuwa jambo hilo mpaka sasa lipo sehemu sahihi na likikamilika wataliongelea

Akizungumza na waandishi Ibraah amesema.................."Tumefanya mazungumzo lakini kikubwa tuwaachie Basata wao ndio wana maamuzi sahihi juu ya hili na namshukuru Mwenyezi Mungu kwasababu tulipofikia ni pazuri''

"Ndani tulichozungumzia ni migogoro iliyopo kati yetu mpaka itakapo kuwa sawa ndio tutaliongea zaidi''