Monday , 12th May , 2025

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu hapo kesho Jumanne Mei 13 kati ya Yanga  dhidi ya Namungo Fc Uwanja wa KMC majira ya Saa ya Saa kumi kamili jioni, Kocha wa Yanga Hamdi Miloud amesema kuwa ni muhumi kushinda mchezo huo ili kuendelea kutengeneza tofauti ya alama zaidi dhidi ya Simba.

Kocha wa Yanga Hamdi Miloud

"Alama moja tunayo tofautiana na Simba haitoshi, tunahitaji kushinda kila mchezo na ndio mlengo namba wa timu yetu wa kuchukua alama tatu. Tuna michezo mitatu pekee za kucheza, ninafuraha kwa kuwa kuna wachezaji wamerejea Uwanjani, Kwahiyo tunaiheshimu Namungo hatupaswi kufanya makosa Kwahiyo ni mchezo muhimu kwetu"- Miloud Hamdi

Namungo hapo kesho watamkosa Mlinzi wao wa kati, Erasto Edward Nyoni kwa sahabu za kikanuni kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.