Monday , 12th May , 2025

Mwanamuziki Foby Official juu ya wasanii kusainiwa na kusimamiwa kazi zao kwenye Records Label.

Picha ya Foby

"Label nyingi za Bongo unaingia ukiwa Msafi unatoka Mchafu. Mifano ipo ndio maana mi niliamuaga kujipambania tu hata kama safari ni ndefu yenye miiba na makorongo kiasi gani ila unafika ukiwa na Uhuru na Amani".

"Kama unaweza kujipambania Jipambanie,Mungu hajawahi kuwa na upande".

Wasanii ambao wametoka kwenye lebo zao mpaka sasa Rich Mavoko, Harmonize, Rayvanny (WCB) Anjella, Killy na Cheed (Kings Music na Konde Music) Yammi (The African Princess) Nedy Music (PKP) Young Killer na Chin Bees (Wanene Entertainment).