Friday , 9th May , 2025

Rapper Nay wa mitego amekanusha taarifa za  kulipwa na chama fulani cha siasa kwa lengo la kuhamia katika chama hicho ambapo taarifa za awali zilisema kuwa msanii huyo amelipwa milioni 100 ili ahamie chama hicho cha siasa.

Sasa kupitia ukurasa wake wa instagram Rapper Nay amejibu taarifa hizo kwa kuandika..............."Mimi Ndo RaisWakitaa Sina Chama Na Sijawai Kua Mwana Chama Wa Chama Chochote In short mimi sio Mwana Siasa. Mimi Ni Sauti Ya Walala Hoi Wenzangu Na Haiwezi Badilika Na Naenjoy kua ivi nilivyo upendo wa watu wangu kwangu una thamani kubwa sana. Haya Nimesikia Dada Angu Mange Kanipiga Promo Ya million 100 Uko banah Haya Uo Wimbo Wenyewe Unatoka JUMATATU Asubuhi Na Mapema''

 

Ikimbukwe kuwa Rapper Nay hajawahi kuweka wazi chama chake licha ya kuwa msanii ambaye amekuwa akionekana kuwasemea zaidi wananchi jambo ambalo wengi hutafsiri kuwa ni msanii wa chama cha upinzani