
JKT Queens vs Simba Queens
Mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 10 jioni una nafasi kubwa ya kuamua ubingwa wa ligi ya Wanawake msimu huu wa 2024-2025 ikiwa imesalia michezo 4 ligi hiyo kutamatika .
JKT Queens wanaongoza ligi kwa alama 38 wakiwa wamecheza jumla ya michezo 14 idadi sawa na Simba Queens anayeshika nafasi ya pili akiwa na alama 37
Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliowakutanisha wababe hao wa ligi ya wanawake ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 ,Simba Queens walitangulia kwa bao la Elizabeth Wambui na baadae Donisia Minja akawasawazishia JKT Queens.