Monday , 5th May , 2025

Sakata la dabi lilipofikia sasa hivi bodi ya ligi ikitoa ratiba yamechi na timu zote zikapewa taratibu za mechi na Yanga asipotokea uwanjani atakuwa hana sehemu ya kujitetea.

Eng Hers Said - Rais wa Klabu ya Yanga

Chombo cha kwanza ambacho Yanga walihisi watapata haki yao (Mamlaka ya usuluhishi ya soka CAS) kimewarudisha kwenye mamlaka za ndani za soka (TFF) ili kukamilisha taratibu zote muhimu zinazohitajika.

“Naona Yanga walipofikia wameona wasifuate taratibu na kanuni zozote ilikutafuta usuluhishi wa mgogoro wao na Mamlaka za soka hapa Nchini wameamua “Liwalo na Liwe”

“Ukisoma kwa umakini barua ya Klabu ya Yanga kuhusu kupinga agizo la CAS wameomba nguvu ya mashabiki zao “wananchi” ili waweze kupambania kwa kile wao wanachokiita haki” – Ibra Kasuga