Wednesday , 23rd Apr , 2025

Instagram imezindua rasmi app mpya ya ku-edit video iitwayo Edits, ambayo lengo lake ni kuwasaidia watengeneza maudhui kuunda video za kuvutia kwa njia rahisi zaidi.

 

Edits inakusaidia kwenye nini labda/ au imeleta utofauti gani ukilinganisha na Apps nyingine za ku-edit video:-

- Kupangilia video yako kwenye namna rahisi zaidi (kwenye mfumo utakaoleta stori ya kuvutia)
- Kurekodi maudhui kwa maana ya ku-shoot 
- Ku-edit video ambapo pia inafanyika kwenye Apps nyingine.

Faidi zipi utazipata endapo utatumia Edits

- Uwezo wa kuondoa background kwenye video yako, kwa maana ya kile kinachoonekana nyuma ya video yako na kuweka utakachokipenda wewe.
- Kile unachokitamka kuwa kwenye mfumo wa maandishi moja kwa moja (automatic captions)
- Mfumo wa akili unde ambao unakuwezesha kubadilisha picha kuwa kwenye mfumo wa Video.
- Inakupa taarifa kuhusu mwenendo wa content yako mtandaoni kwa maana ya insights

Kuanzishwa kwa Edits kutokea kampuni ya META ni kama jibu la CapCut ambayo inamilikiwa na Kampuni ya ByteDance kwa kile wanachodai kwamba ikitokea TikTok imefungiwa nchini Marekani basi moja kwa moja watumiaji wa Capcut wahamie kwenye Edits

NB: CapCut na TikTok zote zinamilikiwa na kampuni moja ambayo ni ByteDance, na Edits na Instagram zote zinamilikiwa na kampuni moja ambayo ni META ndiyo maana ukitaka kujiunga kwenye App ya Edits itahitaji taarifa zako za Instagram.