
Jadon Sancho na Cole Palmer
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alijiunga na Chelsea kwa mkopo mwezi Agosti katika mkataba ambao ulijumuisha kipengele cha kumnunua kati ya £20m na £25m, endapo klabu hiyo ya London itamaliza angalau nafasi ya 14 kwenye Premier League msimu huu.
Chelsea wanashika nafasi ya nne, huku kukiwa na mechi tisa mkononi. Hata hivyo, kwa mujibu wa Athletic, kuna vyanzo vinavyofahamu kuhusu mkataba huo kwamba kuna kipengele kinachoiruhusu Chelsea kumrudisha Sancho Old Trafford mradi tu wailipe United £5m kama fidia.
Chelsea hapo awali walisisitiza kuwa hawafikirii kumuachia Nyota huyo lakini shaka imeanza baada ya Sancho kutokuwa na mwenendo nzuri Stamford Bridge akiwa amechangia asisti moja pekee katika mechi 18 tangu kufunga goli la mwisho kati ya mabao yake mawili dhidi ya Tottenham Desemba 08/2024.