
Cristiano Ronaldo - Nahodha wa kikosi cha Ureno
“Nataka Ureno ishinde, nataka kutetea Bendera ya Nchi yangu mpaka nitakapo kufa. Nitafurahi sana kama leo tutashinda, hata akifunga mchezaji mwingine tofauti na mimi nitafurahi kwasababu lengo letu ni ushindi”
“Kuhusu Hojlund kufunga na kushangilia kama mimi kwangi siyo tatizo, siyo yeye tu watu wengi wamekuwa wakishangilia kwa staili yangu. Leo nitamuonyesha namna ya kuishangilia nitakapofunga” – Cristiano Ronaldo
Portugal Itashuka dimbani leo kukabiliana na Denmark majira ya saa 4:45 usiku kujaribu kulipa kisasi baada ya kupoteza mchezo wa kwanza ugenini kwa kufunga 1-0 goli lililofungwa na mshambuliaji wa Manchester United Rasmus Hojlund