Tuesday , 11th Mar , 2025

Waziri wa masuala ya kigeni Marco Rubio amesema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya programu zinazofadhiliwa na Shirika la Marekani la Misaada ya Kimataifa (USAID) zitafutwa.

Baada ya tathmini ya wiki 6, serikali ya Trump imeamua rasmi’’ kufuta asilimia 83 za programu za USAID,’’ Rubio aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa X.

Aidha anasema kandarasi 5,200 zilitumia mabilioni ya dola katika njia ambazo hazistahiki, na baadhi ya programu pia zikiumiza maslahi ya Marekani.

Vile vile Rubio amedokeza kuwa walishauriana na bunge, na wanakusudia asilimia 18 iliyosalia ya programu tunazobakisha (takriban 1000) zisimamiwe kwa ufanisi zaidi chini ya Idara ya Jimbo.

Pia hakusita kuhongera wafanyikazi wa taasisi mpya ijulikanayo kama 'Department of Government Efficiency' au DOGE – yenye lengo la kupunguza matumizi mabaya ya fedha za umma na kuongeza ufanisi wa watumishi wa umma kufikia mageuzi haya akiyataja ni ya kihistoria.

Rais wa Marekani Donald Trump alisema mwezi jana kuwa’’ ulaghai ulikuwa mwingi’’ katika utumizi wa mfuko wa USAID Na kuamuru usitishe mipango yake.

Utawala wa Trump unatarajiwa kusitisha misaada ya kigeni iliyosimamiwa na USAID.

Mapema mwezi jana, kupitia mtandao wa USAID ulitoa notisi kuwa wafanyakazi wote waende ‘’mapumziko ya lazima’’ wachache hawajaathirika na tangazo hilo.

Shirika la Marekani la Misaada ya Kimataifa (USAID) lilianzishwa miaka ya 1960 ili kusimamia programu za misaada ya kibinadamu kwa niaba ya serikali ya Marekani duniani kote.