Tuesday , 4th Mar , 2025

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani sambamba na wiki ya maji, wanawake wa Wizara ya Maji wamekuja na mkakati maalumu wa ujenzi wa miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri,

Shule ya sekondari Malimbika iliyopo katika kijiji cha Malimbika wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro imechaguliwa kuwa sehemu ya kufanya uzinduzi wa miundombinu ya kuvuna maji ya mvua. Miundombinu hii itajengwa katika mikoa 8 ya Tanzania Bara.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri, amesema kwamba miundombinu inayojengwa inahusisha vioski vya kuchotea maji, vitako vya kuwekea matenki mawili yenye uwezo wa mita za ujazo 10,000 kwa kila eneo, pamoja na kuweka flushing tanks, mabomba ya kuvuna maji ya mvua na kuyakusanya pamoja na mabomba ya kusambaza maji kwenye maeneo hasa vyooni.