
Naibu Waziri Katambi msibani
Huku mlango ukifungwa na kufuli kwa nje.
Katambi amefika kwenye msiba huo leo machi 3, 2025 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Shinyanga, ambapo amesema Ofisi ya Waziri Mkuu inatoa pole juu ya msiba huo na kwamba wataendelea kushirikiana na familia ya marehemu pamoja ili kuona nanma ya kulijengea kaburi lake.
"Poleni sana ndugu zangu kwa msiba huu na kifo cha mwanamke huyu kina uwalakini licha ya kukutwa viungo vyake vipo, lakini utata unakuja nani alifunga kufuli kwa nje, hivyo kazi hii ya uchunguzi tunaliachia Jeshi la Polisi litakuja na majibu, Waziri Ridhiwani Kikwete nimempa taarifa juu ya tukio hili anawapa pole sana, na mimi nitawapatia mkono wa pole ili kusaidia mahitaji mbalimbali ya hapa msibani ikiwamo kununua chakula,"ameongeza Katambi.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbino Manispaa ya Shinyanga Penina Ezekiel, amesema kifo cha mwenzao kimewapa mashaka kuwa kipindi hiki cha uchaguzi maisha yao yapo hatarini na ameiomba serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, kuwahakikishia usalama wao katika kipindi hiki cha uchaguzi, ili wasiuawe na kukatwa viungo vyao, huku akiomba kaburi la mwenzao lijengewe kwa ajili ya usalama zaidi lisije fukuliwa na kuchukuliwa viungo vyake.
Tukio hilo limebainika Machi 2 mwaka huu 2025, baada ya majirani kuhisi harufu kali, ndipo walipotoa taarifa kwa uongozi wa kijiji, ambao nao ulilazimika kuvunja dirisha ndipo walipomuona mwanamke huyo akiwa amelala kitandani huku mwili wake ukitoa harufu kali.