
Mikel Arteta - Kocha wa Kikosi cha Arsenal
The Gunners walipoteza mwelekeo zaidi baada ya wikendi iliyopita kupoteza mchezo 1-0 dhidi ya West Ham huko Emirates.
Timu tatu pekee katika historia ya Ligi Kuu zilipitwa alama 11 au zaidi kisha zikatwaa ubingwa mwishoni mwa msimu. Arsenal bado wana mchezo mmoja mkononi huku wakiwa na mchezo wa marudiano dhidi ya Liverpool huko Anfield tarehe 10 Mei lakini Arteta yeye anaamini kuwa timu yake itasalia kwenye mbio za ubingwa.
"Kimahesabu inawezekana, tunaweza kuziba pengo la alama lililopo na tuna mechi moja mkononi. Ugumu ni mkubwa, ikiwa utashinda Ligi ya Premia kwa hali tuliyo nayo itabidi tufanye kitu ambacho hakuna mtu mwingine amefanya katika historia ya Ligi Kuu."-Mikel Arteta