Tuesday , 25th Feb , 2025

Kocha wa Liverpool Arne Slot anaamini mshambuliaji wake Mohamed Salah atawania tuzo ya Ballon d'Or mwaka huu kutokana na kiwango chake bora na endapo Liverpool itashinda kombe la EPL na UEFA msimu huu.

Arne Slot na Mohamed Salah

Mmisri huyo amefunga magoli 30 katika mashindano yote msimu huu huku akihusika katika magoli 40 ikiwa ni pamoja magoli na assists katika michezo 49.

Slot anaamini kuwa Liverpool wanahitaji kushinda kombe ili kuhakikisha Salah anapata nafasi nzuri zaidi ya kushinda Ballon d'Or mwaka huu.

“Nadhani, kwa ujumla, mtu anayeshinda Ballon d’Or anahitaji kushinda kitu pia, kwa hiyo ni changamoto kubwa ambayo iko mbele yetu na mbele yake.

Sisi kama timu tukiweza kushinda taji, atakuwa na nafasi nzuri zaidi kushinda Ballon d'Or."-Arne Slot Kocha wa Liverpool