Monday , 24th Feb , 2025

Promota wa Daniel Dubois Frank Warren amesema pambano la marudiano kati ya Dubois dhidi ya Oleksandr Usyk bado lipo licha ya mwingereza huyo kushindwa kupanda ulingoni Jumamosi iliyopita baada ya kuugua ghafla

Daniel Dubois

Dubois mwenye umri wa miaka 27 alilazimika kujiondoa katika kutetea mkanda wake wa IBF  dhidi ya Joseph Parker wa New Zealand nchini Saudi Arabia siku ya Jumamosi kwa sababu ya ugonjwa lakini pambano  dhidi ya Usyk mshindi wa mkanda wa  WBO, WBA na WBC bado lipo

Dubois dhidi ya  Usyk walipigana Agosti 2023 na Usky kufanikiwa kushinda kwa raundi 9 na baadaye Dubois akitangazwa kuwa bingwa wa IBF Juni 2024 baada ya Usyk kushindwa kuutetea mkanda huo

Kwa upande mwingine  Usyk alipambana na  Tyson Furry na kushinda mkanda WBO,WBC, WBA na kuwa bondia wa kwanza wa uzani wa juu kumiliki mikanda minne mikubwa katika uzani huo