
Papa Francis
Taarifa imeeleza kuwa hali ya Papa Francis mwenye umri wa miaka 88 bado ni mbaya, lakini tangu usiku wa kuamkia jana Februari 23 hajapata zaidi matatizo ya awali ya upumuaji yaliyokuwa yakimsumbua, huku akiendelea na huduma
Papa Francis ambaye amelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki moja sasa jana alishiriki misa takatifu pamoja na wale ambao wamekuwa wakimuuguza katika chumba maalum alicholazwa katika hospitali ya Gemelli mjini Roma.