
Rais Samia Suluhu Hassan
Pia Rais Dkt Samia amemuagiza Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa kupeleka kiasi cha shilingi milioni 240 kwa ajili ya maboresho zaidi ya kitengo hicho Ili iweze kutoa huduma za kitabibu za matibabu hayo.
Rais Dkt Samia ameyasema hayo katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Tanga.
"Nataka niwaambie kutokana na ujenzi wa hospitali hii hauna viwango vya wilaya ni viwango vya ngazi ya mkoa hivyo namuagiza Waziri Mchengerwa kuipandisha hadhi iweze kutoa tiba ya mifupa kutoka na kwamba kwanza ipo katika eneo la barabara ambazo kuna uwezekano wa uwepo wa ajali lakini na huduma hizi za kibingwa haziwezi kupatikana kila mahali "alisema Rais Samia.
Aidha katika hatua nyingine alisema kuwa uwepo wa hospitali hiyo umeweza kusaidia kuhudumia wajawazito 900 toka ilipoanza kutoa huduma na kati Yao 300 waliweza kupatiwa huduma ya dharura ya upasuaji.
"Ambapo kama hospitali hii isingekuwepo ina maana wajawazito hao wangepelekwa rufaa katika hospitali ya Bombo na wengine wangeweza kupoteza maisha kutokana na changamoto ya umbali wa huduma lakini Sasa mmeweza kuokoa vifo vya wamama wajawazito na watoto"alisema Rais Samia.
Hata hivyo Rais Samia alisema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo Kwa kadiri ya ilivyopangwa kwenye maeneo mbalimbali nchini hivyo wananchi waendelee kuwa na Imani na serikali yao kwani hakuna serikali duniani ambazo zitaweza kumaliza changamoto zote Kwa wakati mmoja.
Vile vile alisema kuwa Kwa sasa serikali Haina dhamira ya kuongeza maeneo mapya ya utawala bali wataendelea kuboresha yaliyopo Ili yaweze kutoa huduma karibu na wananchi zikiwa ni zenye ubora.
Kwa upande wake Waziri wa Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa alisema kuwa Serikali imeweza kutoa kiasi cha sh Tril 1.2 Kwa ajili ya maboresho mbalimbali kwenye sekta afya
"Kwa mkoa huu wa Tanga tumeweza kuleta kiasi cha sh Bil65.6 Kwa ajili ya sekta ya afya ambazo zimeweza kujenga na kukarabati hospitali 10 zilizopo katika ngazi za wilaya sambamba na ujenzi wa vituo vya afya vipya 18 kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huo.alisema Waziri Mchengerwa.